Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, watu wa Italia waliandaa maandamano makubwa ya kupinga vitendo vya jinai inayofanywa na Israel huko Ghaza, maandamano ambayo yamevutia hisia kubwa, umati wa watu mbalimbali kutoka kila pembe ya nchi ulijumuika katika maandamano hayo, zikiwemo familia nyingi zilizoandamana na watoto wao jambo linaloashiria kuwa maandamano hayo yalikuwa ya amani.
Waandamanaji walikuwa wameshika bendera zenye ujumbe kama huo na walikuwa wakipaza sauti huku wakisema: “Komesheni mauaji ya halaiki, komesheni kushirikiana katika mauaji ya halaiki!”
Kwa mujibu wa waandaaji wa maandamano hayo, takriban watu 300,000 walishiriki katika maandamano hayo yaliyoandaliwa na chama cha upinzani cha mrengo wa kushoto nchini Italia, waliitaka serikali ichukue msimamo wa wazi kuhusiana na suala la Ghaza.
Maoni yako